Tangazo: Mahafali Shirika la Elimu Kibaha

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha Dkt. Cyprian Mpemba anatangaza kuwepo kwa  Sherehe za mahafali ya pamoja yatakayofanyika tarehe 26 Septemba,2015.

Aidha, mahafali haya yatashirikisha  Sekondari ya Kibaha,Shule ya Sekondari Tumbi, Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha ,Shule ya Msingi Tumbi na Chuo cha Maendeleo ya jamii KFDC.

Sherehe zitafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibaha kuanzia saa 2 hadi saa 9 mchana.

Nyote mnakaribishwa