Tangazo: Shirika la Elimu Kibaha laadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma 2016 kwa kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi na watumishi.

Shirika la Elimu Kibaha laadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi na watumishi.Tarehe 17 na 18 Juni,2016 Watumishi wa Shirika la Elimu Kibaha walipata fursa ya kuuliza maswali yahusuyo Utumishi wa Umma na walipatiwa majibu ya maswali hayo.

Leo tarehe 22, Juni,2016 na kesho tarehe 23 Juni,2016 wananchi watapata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu huduma zinazotolewa na Shirika la Elimu Kibaha na kupatiwa majibu ya maswali na kero walizonazo.


Imetolewa na : Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

                           Shirika la Elimu Kibaha