Tangazo: KAMBI YA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO LA MGONGO WAZI NA VICHWA KUJAA MAJI

KAMBI YA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO LA MGONGO WAZI NA VICHWA KUJAA MAJI

 Kutakuwa na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye tatizo la mgongo wazi (Spinal Bifida) na vichwa kujaa maji (Hydrocephalus) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani (Tumbi). Zoezi hilo litaendeshwa na Madaktari kutoka taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) na madaktari wa Tumbi Hospital. Zoezi litakuwa la siku TATU; tarehe 12/09/2016-14/09/2016. Wagonjwa wataanza kupokelewa kuanzia Tarehe 11/09/2016 tatika Hospitali ya Tumbi. Wazazi/walezi wenye watoto wenye matatizo hayo mnaombwa kuwaletea watoto wapate tiba.

Mawasiliano;

Dr. Kiwelu 0762060880

Dr. Msangi 0719480310

Dr Dattan 0713601478

       Asanteni.