Tangazo: FURSA YA KUPATA CHUMBA CHA BIASHARA

 

KEC LOGOSHIRIKA LA ELIMU KIBAHA

               

 


FURSA YA KUPATA CHUMBA CHA BIASHARA

ENEO LA “GREEN PARK” (JAVISCO) TUMBI

 

Shirika la Elimu Kibaha linawakaribisha watu wote wenye nia na uwezo wa kujenga chumba cha Biashara  katika eneo la “Green Park” lililopo Tumbi kwenye ardhi ya  Shirika la Elimu Kibaha.

Fomu za maombi zinapatikana kwenye jengo la Ofisi Kuu ya Shirika la Elimu Kibaha, chumba Namba 22. Gharama ya maombi ni Shilingi 20,000 (elfu ishirini tu).

Mwombaji anaweza kukagua masharti ya fursa hii na kupewa maelezo mengine atakayohitaji kabla ya kulipia gharama ya maombi.

Maombi yaliyo kwenye bahasha zilizofungwa madhubuti, yawe yamewasilishwa Ofisi Kuu ya Shirika la Elimu Kibaha, chumba Namba 22, kabla au ifikapo saa 4.00 asubuhi, siku ya Alhamisi tarehe 28.12.2017

 

KARIBUNI WOTE

 

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu

Shirika la Elimu Kibaha