Kaimu Mkuu wa Maktaba ya Umma Kibaha, Bw. Silvernus Nyoni akiwa na watumishi wa Manispaa ya Kibaha ambao wamefanya ziara ya siku moja ya kujifunza usimamizi wa Maktaba.
Bw. Silvanus Nyoni akitoa mafunzo kuhusu masuala ya maktaba kwa watumishi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha waliotembelea Shirika la Elimu Kibaha.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Robert Shilingi akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Juma Messos wakati alipotembelea Banda la Shirika la Elimu Kibaha kwenye Viwanja vya John Malecela jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Shiika la Elimu Kibaha katika maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane 2025 yaliofanyika Viwanja vya John Malecela jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Serikali mkoani Pwani wakiwa wamejitokeza kwa wingi tarehe 02/04/2025 kushiriki unziduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2025 katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.
Watoto wa halaiki wakifanya zoezi la upigaji kura ikiwa ni sehemu ya kuwakumbusha Watanzania kwamba mwaka huu 2025 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, mkimbiza Mwenge (kushoto) tayari kwa kuanza mbio katika Mkoa wa Pwani. Tukio hili lilifanyika katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.