Wigo

Shule Ya Sekondari Kibaha Wasichana

                   SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA KIBAHA

HISTORIA FUPI YA SHULE

 1. UTANGULIZI

  Shule hii ilianza rasmi mwaka 2008 ikiwa na wanafunzi 80 mikondo 2 kidato cha I.  Sasa shule ina wanafunzi 320 kidato cha kwanza hadi cha nne na mikondo 8.   

   

 2. WAFANYAKAZI

  Shule ina jumla ya wafanyakazi 32 miongoni mwao walimu ni 28 na wasio walimu ni 04.  Walimu wanne (04) wapo masomoni na waliopo kazini ni 24.

   

 3. MIUNDO MBINU

  Shule ina jengo la utawala lenye ofisi za idara mbalimbali za masomo na jengo la madarasa lenye vyumba 8 na ofisi  

   4. TAALUMA

 1. Ufaulu katika mitihani ya Taifa (CSEE) kwa miaka mitatu ilikuwa kama ifuatavyo:


  1. ZAWADI KATIKA TAALUMA

   Mwaka 2013, shule ilipata vyeti  vitatu kutokana na kuwa na matokeo mazuri


 1. CERTIFICATE OF OUTSTANDING PERFORMANCE IN FTSEE 2013

 • Cheti hiki kilitolewa na Mkaguzi Mkuu wa Kanda ya Mashariki kwa shule kuwa miongoni mwa shule tatu za Kata bora katika Kanda ya Mashariki.

   

 1. CERTIFICATE OF RECOGNITION

 • Cheti hiki kilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa kuwa shule ya Kata ya kwanza katika Halmashauri katika matokeo ya kidato cha Nne 2013


 1. CERTIFICATE OF RECOGNITION

 • Cheti hiki kilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha kwa kutambua matokeo mazuri ya shule kwenye Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Pili, 2013 kwa kuwa shule ilikuwa ya pili Kikanda katika kundi la Shule za Kata.