Habari
MHE. SELEMANI JAFO AFURAHISHWA KWA SHULE YA KIBAHA SEKONDARI KUWA YA KWANZA KITAIFA KATIKA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA
MHE. SELEMANI JAFO AFURAHISHWA KWA SHULE YA KIBAHA SEKONDARI KUWA YA KWANZA KITAIFA KATIKA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA
Tarehe 15 Julai,2018
Waziri wa Tamisemi Mhe. Selemani Jafo afurahishwa kwa Shule ya Sekondari Kibaha kuwa ya kwanza kitaifa katika mitihani ya kidato cha sita ambapo shule hiyo imekuwa ya kwanza kitaifa. Akiongea na wanafunzi wa Shule hiyo katika bwalo la Shule Mhe. Jafo amesema “nimefurahishwa sana na matokeo ya kidato cha sita,nilipofanya ziara mwezi januari waliniahidi watakuwemo katika tatu bora na sasa wamekuwa wa kwanza kitaifa haya ni mafanikio makubwa sana kweli wameonesha kuwa ni mashujaa wa kibaha.
Awali akitioa taarifa mbele ya Mhe. Waziri Jafo , Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha bw. Robert Shilingi amesema Shule ya Sekondari Kibaha pamoja na ufaulu mkubwa ina changamoto ya miundo mbinu pamoja na walimu kutopanda madaraja kwa muda mrefu. Amesema walimu wa Shule ya Sekondari wameendelea kufundisha kwa bidii mpaka kufikia hatua hiyo kubwa kitaifa.
Naye Mkuu wa Shule bw. Chrisdom Ambilikile amewashukuru walimu wa Shule yake kwa kujitoa na kuhaklikisha shule ya Sekondari Kibaha inakuwa ya kwanza kitaifa katika mitihani ya kidato cha sita 2018.
Shule ya Sekondari ilianzishwa mwaka 1965 tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma, viongozi wengi wa kitaifa wmeasoma katika shule hii kwa sasa inaendelea kuwa mojawapo ya shule ya wanafunzi wenye vipaji maalum nchini Tanzania.