Dira, Dhima na Maadili

DIRA

Shirika la Elimu Kibaha lina malengo ya kuwa kituo bora katika kutokomeza umasikini, ujinga na maradhi.

DHIMA

Shirika la Elimu Kibaha limejitolea kutoa huduma bora za kijamii kupitia utumiaji mzuri wa rasilimali, kujenga uwezo na utawala bora katika njia jumuishi ili kuboresha hali ya Maisha ya watu.

MAADILI MAKUU.

Shirika la Elimu Kibaha, linazingatia maadili yafuatayo:-

i.Kupunguza Umasikini

ii.Utawala bora (demokrasia, usawa, utawala wa sheria, uwazi na uwajibikaji);

iii.Utoaji mzuri na bora wa huduma za kijamii na kiuchumi

iv.Usawa katika hali ya afya na huduma ya afya;

v.Usawa katika hali ya elimu;

vi.Kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu ;

vii.Ufanisi wa gharama (thamani ya fedha) na ubora;

viii.Kuridhika kwa mteja na mtoa huduma;

ix.Uwazi na uwajibikaji;

x.Umiliki na ushirikiano katika huduma za afya, elimu, maendeleo ya jamii, na

xi.Kufuatilia na kutathmini utendaji wa kazi katika huduma za afya, elimu na maendeleo ya jamii ili kuhakikisha uwajibikaji na uzingatiaji wa viwango na sera za kitaifa.