Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Serikali mkoani Pwani wakiwa wamejitokeza kwa wingi tarehe 02/04/2025 kushiriki unziduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2025 katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.
Watoto wa halaiki wakifanya zoezi la upigaji kura ikiwa ni sehemu ya kuwakumbusha Watanzania kwamba mwaka huu 2025 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, mkimbiza Mwenge (kushoto) tayari kwa kuanza mbio katika Mkoa wa Pwani. Tukio hili lilifanyika katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasha Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2025 katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdori Mpango akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2025 katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani. Uzinduzi umefanyika tarehe 02/04/2025.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Elimu Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Dkt. Emmanuel Shindika (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Elimu Kibaha.