Habari

Shirika la Elimu Kibaha lapata hati safi kwa ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2020/2021


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Bw. Robert Shilingi, jana Jumanne tarehe 21/06/2022 amefanya mkutano na watumishi wote wa Shirika la Elimu Kibaha.

Akizungumza na watumishi hao, Bw. Shilingi ameeleza mafanikio ya Shirika kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na matarajio ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Shirika la Elimu Kibaha kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

“Kwa mwaka wa fedha uliopita 2020/2021 tulifunga hesabu kwa wakati, ukaguzi ulifanyika vizuri na matokeo ya ukaguzi huo yameonyesha kuwa Shirika limepata hati safi, hongereni watumishi kwa kuwezesha jambo hili.” Alisema Bw. Shilingi.

Akiendelea kuungumza katika mkutano huo, Bw. Shilingi ameeleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022 tumetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mabweni matatu katika shule ya sekondari ya wasichana Kibaha wenye thamani ya Tsh. 240,000,000 kutoka Serkalini kupitia program ya EP4R; ujenzi wa vyumba vipya vitatu vya madarasa na ukarabati wa majengo ya shule ya msingi Tumbi wenye thamani ya Tsh.281,000,000 kutoka Serikalini.

Pia miradi mingine ni ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari ya wasichana Kibaha wenye thamani ya Tsh. 40,000,000 kutoka Serikalini; ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari ya Tumbi wenye thamani ya Tsh. 40,000,000 kutoka Serikalini kwa fedha ya UVIKO 19; ujenzi wa madarasa na ofisikatika shule ya watoto wadogo Tumbi wenye thamani ya Tsh. 30,000,000 kutoka kwenye mapato ya ndani ya Shirika, ujenzi wa chumba cha darasa katika chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha.”

Wakati huo huo, watumishi wa Shirika la Elimu Kibaha, walipata tarifa ya kuidhinishwa kwa muundo wa maendeleo ya watumishi na pia kusikia mipango ya maendeleo ambayo Shirika linatarajia kuifanya kwa mwaka mpya wa fedha 2022/2023 ambayo ni ukarabati wa chuo cha maendeleo ya wananchi Kibaha kwa kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia; kukarabati shule ya Sekondari ya Tumbi; ukarabati na upanuzi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha ili kuongeza idadi ya kozi zinazotolewa; na kuanzisha bustani ya wanayamapori ‘Zoo Park’.

Mkutano huo ni utaratibu wa uongozi wa Shirika wa kuwatoa taarifa juu ya utekelzaji wa shughuli mbalimbali na kupokea maoni ya watumishi ili kuboresha utekelezaji huo.