News

SHULE ZA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA ZAPATIWA UFADHILI WA WA UJENZI WA BWENI PAMOJA NA


Na Lucy Simindu Kibaha

Taraehe 23 Julai,2020

Kwa upande wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha imepatiwa shilingi milioni 80 kwa ajili ya kujenga bweni ambalo litakuwa uwezo wa kuchukua wanafunzi 40 ikizingatiwa shule hii imesajiliwa kuwa Shule ya Bweni na hii itawezesha wanafunzi kupata muda mzuri wa kujisomea vizuri.

Hata hivyo Uongozi wa Shule ili kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kujisomea zaidi wameweka mpango wa Wanafunzi kupatiwa chakula cha mchana . Mpango huu unafadhiliwa n Shirika la Elimu Kibaha,Wazazi pamoja na wasweedish waliowahi kufundisha kwenye Shule za Shirika na maeneo mengine.

Shule ya msingi Tumbi iliyojengwa mwaka 1966 ambapo kwa sasa ina miaka 54, imetengewa shilingi million i60 na mardi PFR kwa  ajili ya ujenzi wa madarasa matatu. Kiufupi Shule hii ni nikongwe madarasa karibu yote yanatakiwa kukarabatiwa na kujengwa upya.

Chuo cha KFDC ambayo nayo ni kongwe, imeezekwa kwa asbestos ambayo ina madhara kwa binadamu. Chuo hiki nacho kinatafutiwa ufadhil na kuezekwa upya pamoja na ukarabati wa miundo mbinu kama karakana na meneo mengine. Hata hivyo Shirika la Elimu Kibaha tayari kwa kutumia fedha za ndani imeanza ukrabati katika Jengo la Utawala na baadhi ya madarasa.