Wigo

Utafiti na Maendeleo

Utafiti na Maendeleo ni moja kati ya Idara tatu zilizo chini ya Kurugenzi ya Maendeleo ya Jamii iliyoanzishwa Julai, 2010. Idara hii inafanya kazi na watu katika Kata nane (8) na Mitaa 34 katika mji wa Kibaha kwa kuendesha vikao kwa lengo la kutambua mahitaji yao kwa ujumla na mahitaji maalumu kwa makundi ya watu maalumu wanaoishi katika mazingira hatarishi wakiwemo watoto, wazee na wajane.

Malengo ya Idara

Kufanya tafiti na tathmini kuhusu mahitaji ya watu katika jamii inayozunguka Shirika la Elimu Kibaha ili kuboresha maisha yao.

Kuratibu huduma za ugani kwa wakulima katika maeneo yalioko karibu na Shirika

Kuratibu mafunzo ya kozi fupi ikiwemo ujasiriamali katika mji wa Kibaha, mkoani Pwani.

Kuratibu ubunifu na ugunduzi wa mashine rahisi kwaajili ya teknolojia inayofaa na kusambaza kwa wadau

Shughuli za Idara

Ikiongozwa na Meneja wa Utafiti na Maendeleo, shughuli za Idara hii ni pamoja na:

Kufanya tafiti kulingana na rasimu za mipango ya utafiti zilizoandaliwa, kuandaa taarifa za utafiti na kusambaza taarifa hizo kwa wadau

Kufanya tathmini kuhusu mahitaji ya jamii ikiwemo mahitaji ya mafunzo kwa jamii ili kuboresha maisha yao.

Kufanya ufuatiliaji kwa wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi cha Kibaha na kuandaa taarifa. 

Kuhudumia na kusaidia makundi ya watu wanaoishi katika mazingira hatarishi katika jamii wakiwemo watoto, watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na UKIMWI, wazee na wajane.

Kufanya shughuli za ugani hususan katika kilimo na mifugo kwa jamii inayozunguka Shirika

Kuratibu mafunzo ya kozi fupi kwa makundi mabalimbali ya wanainchi wa Kibaha na inje ya Kibaha.

Kutumia teknolojia kutengeneza zana na kuzitumia ipasavyo na kuzisambaza kwa jamii ili kuboresha uzalishaji

Vitengo vya Utafiti na Maendeleo

Idara hii imegawanyika katika vitengo vine (4) kama ifuatavyo

Shughuli za Utafiti

Mafunzo ya kozi fupi

Huduma za ugani

Ubunifu na Ugunduzi

Shughuli za Utafiti 

Kupitia Idara ya Utafiti na Maendeleo, Kurugenzi ya Maendeleo ya Jamii ina wajibu wa kuratibu shughuli za utafiti katika Shirika. Timu ya watafiti yenye wafanyakazi kumi (10) wenye ujuzi wa masuala ya utafiti imeundwa ili kufanya tafiti mbalimbali katika sekta mbalimbali ikiwemo maendeleo ya jamii, elimu, na huduma za afya. Idara ina shirikiana na taasisi zingine ndani na inje ya Tanzania kufanya tafiti.

Mafunzo ya Kozi Fupi

Kozi fupi zinaendeshwa kulingana na mahitaji ya wadau na kwasababu hiyo mafunzo ya kozi fupi yanaendeshwa kulingana na mahitaji ya jamii. Baadhi ya kozi zinazotolewa ni hizi:

Ujasiriamali

Ufugaji kuku

Ufugaji nyuki

Ufugaji samaki

Ufugaji mifugo

Kilimo cha uyoga

Upishi na huduma za hoteli

Huduma kwa wateja

Mafunzo ya Udereva

Huduma za ugani

Idara ya Utafiti kwa kushirikiana na Idara ya Mashamba ya Mfano inahudumia wakulima wadogo kwa kutoa ushauri katika kuboresha kilimo, ufugaji mifugo na nyuki.

Ubunifu na Ugunduzi

Kwa kushirikiana na Idara ya Mafunzo (Chuo cha Maendeleo ya Wananchi) na SIDO juhudi zinafanywa kutengeneza mashine na zana rahisi ambazo zita boresha teknolojia kwa wakulima wadogo. Mashino hizo ni pamoja na mashine ya kuchanganyia chakula cha mifugo, toroli, mashine ya kutengenezea matofali, kiatamizi.