Wigo

Hospital ya Rufaa ya Mkoa Tumbi

Hospitali ya Teule ya Rufaa ya Mkoa- Tumbi ilianzishwa kama Kituo cha Afya mnamo mwaka 1967, ikiwa na vitanda 35. Mwaka 1979 Kituo cha Afya kilipandishwa hadhi na kuitwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Kibaha.
Mnamo tarehe16.02.1996, Hospitali ilitunukiwa jina la “Hospitali Maalum ya Tumbi”.Mwaka 2008, Hospitali Maalum ya Tumbi ilikuwa na vitanda 253 kwa ajili ya kulaza wagonjwa.   Hospitali Maalum ya Tumbi, ndiyo kubwa katika wilaya ya Kibaha, hivyo ilitunukiwa hadhi ya kuwa  Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani mwaka 2011 ikiwa na vitanda 281. Inahudumia idadi kubwa ya watu 1,110,917 katika mkoa wa Pwani ikiwa inapokea wagonjwa 400-500 kwa siku.
Dhamira: kuwa kituo cha ubora katika utoaji wa huduma za afya na mafunzo ili kukidhi mahuiatji ya jamii
Dhima:  Kutoa huduma bora na gharama nafuu kuimarisha, kuzuia, kutibu, kurekebisha, mafunzo na huduma tulivu na faraja afya kwa jamii kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
Maadili
Ukarimu: Kukaribisha na kuzungumza na wateja katika namna ya kirafiki
usawa: Utoaji wa huduma za afya kwa jamii kulingana na mahitaji yao bila kujali  rangi, jinsia, kabila au taifa.
Uwajibikaji: kuwajibika kwa wateja, wanajamii na wadau wengine katika utoaji wa huduma za  Afya.
Uwazi:  kutenda kwa uwazi na ukweli katika kila kitu.
kijamii: kutambua na kuheshimu umuhimu wa mahitaji ya huduma za afya katika jamii.

ushirikiano: kufanya kazi pamoja kwa kushirikiana, na kutambua kwamba juhudi zetu pamoja zitapelekea mafanikio kwa pamoja

MAELEZO YA HOSPITALI

Hospitali hutumika kama ngazi II na III pia inapata wagonjwa kutoka wilaya zote na mikoa ya jirani. Timu ya usimamizi wa hospitali ina wanachama msingi 12 na ina jukumu la kusimamia shughuli zote za kila siku na inaongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali katika Shirika la Elimu Kibaha.
HUDUMA YA DHARURA
Hospitali iko kando ya barabara ya Morogoro, inapokea 80% ya majeruhi wa ajali zote za barabarani kutokea katika eneo hilo na zaidi ya 8% ya ajali za barabarani  nchini
KITENGO CHA INFUSION
Kitengo hiki kinazalisha lita 240 pia kwa sasa kitengo kina uwezo wa kuzalisha Dextrose 5% 500mls, 250mls, 10% 250 mls, 50% 50 mls, Ringer lactate 500 mls, 500mls dextrose chumvi, chumvi ya kawaida 0.9% ya 500mls na 30% ya 50 mls.

CARE & TREATMENT CENTRE
Kliniki inahudumia  wateja 70-80  kwa siku. Shughuli zake ni pamoja na  matibabu ya VVU / UKIMWI. Katika hospitali ya Tumbi kitengo hiki kilianza Juni 1, 2005

Kliniki hii inatoa ushauri nasaha na kupima, ushauri wa lishe, na uchunguzi pamoja na matibabu yaani utoaji wa tiba ya kurefusha maisha (ARV) kwa wateja wa VVU / UKIMWI na magonjwa ya zinaa.