Wigo

Mashamba Mifano

Mashamba ya Mfano

Idara ya Mashamaba ya Mfano ni moja kati ya Idara zilizo chini ya Kurugenzi ya Maendeleo ya Jamii. Idara hii imegawanyika katika vitengo viwili (2)-Shamba la Mfano la Mazao, na Shamaba la Mfano la Mifugo.

Malengo ya Idara

Kutoa huduma za ugani na mashamba ya mifano ya mazao na mifugo kwa wakulima ili kuinua uzalishaji kwa uwiano wa wanyama na kwa eneo la shamba

Kutoa stadi za kilimo na mifugo kwa njia ya mazoezi kwa vitendo kwa wanafunzi na wakulima ndani na inje ya Shirika.

Shughuli za Idara

Ikiongozwa na Meneja wa Mashamba ya Mfano, shughuli za Idara hii ni pamoja na:

Kugundua na kusambaza teknolojia sahihi kwa wakulima

Kuwapa ekimu wakulima wadogo kuhusiana na uzalishaji mazao na mifugo

Kutathmini mafanikio ya mashamba kila wakati

Kufanya maonesho kuhusu kilimo cha mbogamboga, mazao na ufugaji kwa wakulima wadogo na wanafunzi

Vitengo vya Mashamba ya Mfano

Shamba la Mfano la Mazao

Kitengo hiki kimejikita katika utoaji wa stadi na maarifa kwa njia mbalimbali za mazoezi kwa vitendo kukuza mazao. Mazao mbalimbali yakiwemo ya chakula na biashara, mbogamboga , matunda yanalimwa katika mashamba ya mfano kwenye ukubwa wa Hekali 5 zilizopo kwa sasa.

Shamba la Mfano la Mifugo

Kitengo hiki pia kimejikita katika kutoa stadi na maarifa kwa wakulima wadogo hususani wafugaji na wafugaji tarajali. Shughuli kama vile usimamizi wa mifugo, utengenezaji wa chakula cha mifugo, uansishaji wa malisho ya mifugo vinafanywa katika kitengo hiki.