Wigo

Kibaha Folk Development College

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KFDC) kilianzishwa mwaka 1964 kama Chuo cha Wakulima (Farmers Training Centre) kikiwa ni chombo kimojawapo cha kutekeleza moja ya madhumuni makuu matatu ya kuanzishwa kwa Shirika la Elimu kibaha ambalo ni kukabiliana na adui umaskini kwa wananchi toka mikoa ya Tanga, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam. Mwaka 1975, Chuo kilibadilishwa jina na kuitwa Chuo cha Maendeleoo ya Wananchi Kibaha. Malengo na shabaha zake ziliendelea kubaki zile zile za kutokomeza umaskini pamoja na kuwa Chuo Mama cha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi Tanzania. Kama Chuo Mama, KFDC, kiliongezewa majukumu ya kufundisha wakufunzi wapya wanaojiunga na vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (VMW) falsafa na njia za kumfundisha mtu mzima. Kuendesha Warsha na semina kwa walimu na watumishi wa VMW. Warsha na semina zilihusu uboreshaji wa taaluma na utendaji bora wa kazi katika VMW. Mwaka 1992 Chuo kiliacha kuwa na kujumu la kuwa Chuo Mama.


Mafunzo Yanayotolewa na Chuo

Chuo kina uwezo wa kupokea jumla ya wanachuo 200 kwa mwaka. Bweni 128 na kutwa 72. Masomo yanayotolewa katika chuo cha KFDC ni kama yafuatayo:-

 1. Fani ya Kilimo na Mifugo

 2. Fani ya umeme wa majumbani

 3. Fani ya uungaji na uundaji vyuma

 4. Fani ya magari na mitambo

 5. Fani ya ujenzi (useremala, uashi na bomba)

 6. Fani ya ushonaji

 7. Fani ya upishi

Wanachuo pia wanatakiwa kusoma masomo yanayohusiana na fani hizo ambayo ni:-

 • English and communication skills

 • Life skills

 • Entrepreneurship

 • Technical drawing

 • Mathematics

 • Computer science

 • Engineering science

 • French

 • Tourism

 • Quantitative methods.

Chuo pia hutoa kozi fupi ya udereva kwa muda wa miezi miwili na wahitimu hupata vyeti na kupelekwa kwa maafisa usalama barabarani kujaribiwa na hatimaye kupewa leseni.

Chuo hutoa mafunzo maalum (stadi) zinazopendekezwa na Halmashauri za Wilaya kwa wananchi wake. Mafunzo ya namna hiyo hugharimiwa na Halmashauri hizo.

Pamoja na mafuzo hayo Chuo hutoa huduma kwa ukodishaji wa kumbi kwa ajili ya Semina, sherehe nk na utoaji wa chakula na malazi kwa wanasemina hao.

Taratibu za Kujiunga na Chuo

Taratibu za kujiunga na chuo ni kwamba kwanza yanatolewa matangazo kwa kubandikwa kwenye mbao za matangazo kwenye ofisi mbalimbali, katika wilaya ya kibaha na pia kwenye makanisa na misikitini. Anayetaka kujiunga huchukua fomu na baadae kufanya usaili.