Wigo

Shule Ya Msingi Tumbi

Shule ya Msingi Tumbi ni moja kati ya shule zilizopo Halmashauri ya Mji Kibaha katika Mkoa wa Pwani.  Shule ya Msingi Tumbi ni moja ya Shule zilizopo katika Kurugenzi ya Huduma za ELimu katika Shirika la Elimu Kibaha.  Shule ilianzishwa mwaka 1967 na kuandikisha idadi ya wanafunzi ambayo haikuzidi 30.

Shule kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 823 kati yao wavulana ni 405 na wasichana 418.  Vile vile shule ya Msingi Tumbi ina Shule ya Awali yenye jumla ya wanafunzi 87 kati yao wavulana ni 44 na wasichana 43

Hata hivyo shule ya Msingi Tumbi ni moja ya shule za serikali zilizo katika Halmashauri ya Mji Kibaha zinazofanya vizuri kitaaluma na kimazingira pia.