Wigo
Shule Ya Sekondari Tumbi
Shule ya Sekondari Tumbi ni kati ya Taasisi za Shirika la Elimu kibaha. Ipo kilometa 4 kutoka kwenye kitovu cha mji wa halmashauri ya mji Kibaha (Maili Moja) au kilometa moja kutoka katika kijiji cha Picha ya Ndege.
Shule ilianza rasmi mwaka 1999 ikiwa na idadi ya wanafunzi 30 tu, wasichana 13 na wavulana 17 ikiwa na mkondo mmoja (1) na mpaka leo hii shule ina idadi ya wanafunzi 578, ikiwa na wasichana 231 na wavulana 347. Kwa sasa shule ina jumla ya mikondo 16, kwa kila kidato.
Shule ina jumla ya wafanyakazi 43 miongoni mwao walimu wakiwa 37 na watumishi wasio walimu 06. Kati ya walimu hao wenye shahada za uzamili ni 05, shahada 18 na stashahada ni 12.
Shule ya sekondari Tumbi ni ya mchepuo wa sayansi, biashara na maarifa ya nyumbani, hivyo masomo yanayofundishwa katika shule hii ni:
1. CIVICS 2. ENGILSH LANGUAGE 3. KISWAHILI 4. GEOGRAPHY 5. HISTORY 6. BIOLOGY 7. BASIC MATHEMATIC 8. PHYSICS 9. CHEMISTRY 10. COMMERCE 11 BOOK KEEPING 12. FOOD AND NUTRITION
MAFANIKIO YA SHULE KITAALUMA
Taaluma ya shule ya Sekondari Tumbi imezidi kupanda mwaka hadi mwaka kama ifuatavyo:-
MWAKA |
% YA UFAULU |
2009 |
82 |
2010 |
84 |
2011 |
79 |
2012 |
37 |