Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

KAIMU MKURUGENZI MKUU SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA AWAPONGEZA WALIMU KWA MATOKEO MAZURI YA MITIHANI  MWAKA 2024.

Imewekwa: 10 Sep, 2025
KAIMU MKURUGENZI MKUU SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA AWAPONGEZA WALIMU KWA MATOKEO MAZURI YA MITIHANI  MWAKA 2024.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC) amewapongeza watumishi walimu kwa kufanya kazi kwa bidii na kufanikisha matokeo mazuri ya mitihani ya kitaifa ya Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa mwaka 2024.

Katika kutambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi, Shirika la Elimu Kibaha limewakabidhi walimu hao *vyeti vya pongezi* pamoja na *zawadi ya fedha taslimu*.

"Tukio hili limeonesha dhamira ya shirika katika kuendelea kuhamasisha ubora wa elimu kupitia motisha na utambuzi wa juhudi za walimu na wafanyakazi wote walioshiriki kuleta mafanikio haya," amesema Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bw. Sixbert Luziga.

Bw. Luziga amesema mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya walimu, viongozi wa Mkurugenzi ya Elimu na jamii kwa ujumla.

 Pia, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, amewasihi walimu kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta mageuzi chanya ya elimu ndani ya Shirika la Elimu Kibaha na nchi kwa ujumla.

Naye, Kaimu Mkuu wa Kurugenzi ya Elimu, Bw. Jonas Mtangi amewasisitiza walimu kupambana kutafuta alama  A ili kuendelea kupata zawadi.

Aidha, amewasihi walimu kuendeleza ushirikiano ili kuleta matokeo chanya kwa shule zetu za Shirika la Elimu Kibaha.