Habari

BALOZI WA KOREA KUENDELEA KUISAIDIA HOSPITALI YA TUMBI


BALOZI WA KOREA KUENDELEA KUISAIDIA HOSPITALI YA TUMBI

NA LUCY SEMINDU – SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA

Tarehe 16 Juni,2016

Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Balozi. Song Geum-young amesema Serikali yake itaaendelea kuisaidia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi wakati alipokuja leo kutembelea hospitali hii na kuona vifaa tiba na miundo mbinu ambayo Serikali ya Korea ilitoa msaada kwa Hospitali ya Tumbi.

Balozi Song Geum-young ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada kubwa inayoendelea ya kukuza uchumi ili kuweza kufikia uchumi wa kati na amesema Serikali yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania hasa katika Sekta ya afya.

Amefafanua kuwa wamejikita katika kusaidia miundo mbinu ya Hospitali,vifaa tiba ,utoaji wa usahauri wa kitalaam kuhusu huduma ya afya pamoja na kubadilishana uzoefu kwa kuleta Wataalam wa Afya nchini na pia kutoa nafasi kwa baadhi ya Madaktari nchini kwenda Korea kupata mafunzo mafupi yatakayosaidia kuongeza utalaam katika utoaji huduma ya afya.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Bi Chiku Wahdy aliishukuru Serikali ya Korea kwa msaada mkubwa waliotoa kwa Hospitaliya Tumbi i na kwamba wataenedelea kuwa na ushirikiano na Wataalam wa Afya  kutoka Korea.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Afya Shirika la Elimu Kibaha Dr. Bryson Kiwelu, amemweleza Balozi Song kuwa wanatambua mchango wa  Serikali ya Korea kwa hospitali ya Tumbi . Amefafanua  kuwa  Hospitali bado  inakabiliwa na changamoto ya kupokea wagonjwa wengi wanaotokana na ajali za barabarani na kwamba kuna wagonjwa wengi wenye uhitaji wa kipimo cha CT -scan na MRI hivyo mashine hizo zikipatikana zitasaidia kufanya vipimo hivyo kwa urahisi zaidi.

Serikali ya Korea kupitia KOFIH imekwishatoa msaada wa ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto, Jengo la Kitengo cha Mionzi (radiology), vifaa vy tiba vya macho , magari ya wagonjwa na vifaa tiba mbalimbali.