Habari

BODI MPYA YASHIRIKI KATIKA ZIARA YA MAENEO YA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA


Bodi mpya ya Shirika la Elimu Kibaha imeanza kazi yake rasmi kwa kuwa na ziara katika maeneo mbalimbali ya Shirika. Ambapo tarehe 17 Julai kutakuwa na kikao cha kwanza cha Bodi.

Bodi hiyo inayoongozwana Mwenyekiti Profesa Raphael Chibunda ilikuwa ni ziara yenye mafanikio makubwa kwani changamoto  mbalimbali zinazoikabili miradi na maeneo mengineya Shirika yalibainishwa ushauri ya namna ya kutatua changamoto hizo ulitolewa.

Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Chuo cha Uuguzi,Hospitali ya Tumbi,Sekondari ya Kibaha,Shule ya Msingi Tumbi,Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha,KFDC pamoja na Diary Farm.