Habari

CHUO CHA KCHOHAS CHAPATA MAFANIKIO MAKUBWA


CHUO CHA KCHOHAS CHAPATA MAFANIKIO MAKUBWA  

- MAHAFALI KICHOHAS YAFANA

Na: Lucy Semindu - SEK 

Tarehe 2, Agosti,2019 ni siku muhimu sana katika historia ya Chuo cha Sayansi Shirikishi KCHOHAS kwani wanafunzi zaidi ya 300 wamehitimu katika fani mbalimbali za utabibu katika Afya.

Mhe. Koka ameipongeza Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuboresha huduma za Afya ambapo miundo mbinu ya afya imeendelea kujengwa na kuboreshwa.

 Mhe Koka amesema ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kibaha  inayojengwa katika eneo la Lulanzi ni kielelezo cha mafanikio katika upande wa afya nchi nzima.  

Akijibu changamoto mbalimbali zilizotolewa na Mkuu wa Chuo Dkt. Maria Manase na wahitimu Mke Koka amesema changamoto amezisikia na atakuwa mstari wa mbele kuzisema Bungeni ili Serikali iweze kuzitatua.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Maria Manase amemuomba Mhe. Koka kushirikiana bega kwa bega na Chuo cha KCHOHAS ili changamoto ya madarasa,mabweni maabara na na miundo mbinu mingine ya afya  iweze kupata ufumbuzi.

Mgeni rasmi Mhe. Koka aliwatunuku wahitimu zawadi na vyeti vya kuhitimu pamoja na kushiriki katika harambee ya aina yake kwa kukata keki na kulisha keki wageni waalikwa ambapo zaidi ya shilingi milioni moja zilipatikana.

Chuo cha KCHOHAS kina historia ya muda mrefu toka kilipoanzishwa mwaka 1968 ilipoanza kutoa watalaamu wa afya wa  Vijijini mpaka hivi sasa.