Habari
DKT. LUCY SENDI ATAHADHARISHA KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI
DKT. LUCY SSENDI ATAHADHARISHA KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI
7 Aprili ,2016
Na: Lucy Semindu – Shirika la Elimu Kibaha
Mabadiliko ya tabia nchi yana athari kwa uhai wa binadamu kuliko baadhi ya athari ziletwazo na mambo mengine, hayo yameelezwa na Dkt. Lucy Sendi wakati akitoa maada ya mabadiliko ya tabia nchi kwa Menejimenti ya Shirika la Elimu Kibaha leo katika ukumbi wa mikutano wa Shirika.
Akifafanua athari ya mabadiliko ya tabia nchi kwa binadamu Dkt. Lucy Sendi amesema kuwa kati ya miaka ya 1980 hadi 2010 dunia imepitia katika mabadiliko makubwa ya hali ya hewa ambapo kiasi cha joto duniani kimeongezeka.
Aidha, Dkt. Lucy amesema kuwa kuongezeka kwa hali ya joto duniani kunatokana na athari inayochangiwa na shughuli za binadamu kama vile ukataji ovyo wa miti,athari ya moshi unaotokana na magari na viwanda na uharibifu wa mazingira .
Dkt. Lucy amesema vikao mbalimbali vimeshakaa katika ngazi ya Dunia kutafakari athari ya mabadiliko ya tabia nchi na namna athahari hiyo inavyoweza kupunguzwa kwa utunzaji wa mazingira.
Alibainisha kuwa mabadiliko ya tabia nchi athari zake hazionekani kwa haraka lakini jinsi joto linavyoongezeka duniani inaweza kuleta maafa makubwa zaidi kuliko ilivyo hivi sasa. Alitaja baadhi ya athari ni ukame uliokithiri,hali ya hewa kubadilika na kuwa joto sana kiasi cha kuathiri viumbe,mimea na hata uhai wa binadamu.
Mababadiliko ya tabia nchi yana madhara makubwa kwa binadamu na dunia hivi sasa inajitahidi kupambana na madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.