Habari

NAIBU WAZIRI AFYA,MAENDELEO YA JAMII , JINSIA ,WAZEE NA WATOTO ARIDHIKA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA PWANI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

NAIBU WAZIRI AFYA ,MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO ARIDHIKA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA PWANI 

Tarehe: 9/10/2019 Kibaha- PWANI 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na watoto Mhe. Faustine Ndugulile katika majumuisho ya ziara  yake aliyofanya leo tarehe 9/10/2019 katika Hospitali ya ya Tumbi.

Vitengo vilivyotembelewa ni pamoja na OPD, Maabara, Damu Salama, Bohari ya vifaa, Bohari ya dawa ,Wodi ya watoto na Wodi ya Mama na Mtoto pamoja na “mortuary”sehemu ya kuhifadhi miili.

Vitengo vilivyoonekana vimefanya vizuri ni pamoja na Maabara kwa utunzaji mzuri wa myororo wa ubaridi katika majokovu yenye dawa ,sifa hizo pia wamepewa Kitengo cha Damu Salama.

Pia ametoa onyo kali kwa Mkuu wa Bohari ya dawa kwa kuhifadhi dawa kwenye jokovu bovu na kushindnwa kuweka kumbukumbu  ya mnyororo wa ubaridi kwenye jokovu hilo. Kosa lingine ni kushindwa kuweka kumbukumbu ya upokeaji na utoaji wa dawa kwenye kompyuta na ameagiza jambo hilo lirekebishwe.

Hata hivyo ameagiza sampuli za miili hiyo zihifadhiwe ili kama ndugu wakijitokeza iwe rahisi kufanya uchunguzi wa vinasaba “DNA” ili ndugu waweze kufahamu kuwa ndugu yao alifariki na kuzikwa.

Mhe. Ndugulile ametoa vipaumbele vya wizara yake na wanaendelea na maboresho ya Miundo ya Kiutumishi, uboreshaji wa vyumba vya upasuaji ,uboreshaji wa huduma ya Mama na Mtoto ikiwemo ICU ya  wakubwa na watoto.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi ni moja ya Hospitali inayotoa huduma nzuri kwa wanaopata ajali za barabarani.

Imetolewa na:  Lucy Leons Semindu

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano