Habari

MASHRIKIANO BAINA YA MJI WA GOTLAND SWEDEN NA SEK YALETA MAFANIKIO


MASHRIKIANO BAINA YA MJI WA GOTLAND SWEDEN NA SEK YALETA MAFANIKIO


TAREHE 7 FEBRUARI, 2017

NA: Lucy Semindu  SEK

 Shirika la Elimu Kibaha lina ushrikianao na nchi za Scandanvia  ikiwemo Sweden kwa zaidi ya miaka hamsini . Kila mwaka kumekuwa na  desturi ya Watumishi kutoka SEK na Sweden kutembeleana ili kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuongeza tija katika taasisi husika.

Leo Meya wa Jiji la Gotland Sweden na msafara alioambatana nao walitembelea Shirika la Elimu Kibaha kwa lengo la kubadilishana uzoefu na pia kuangalia miradi waliyowahi kufadhili katika mashirikiano hayo yanayoendelea.

Meya huyo wa Jiji la Gotland Sweden alipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Dkt. Cyprian Mpemba ambaye alimweleza kuwa mashirikiano yalioyopo kati ya SEK na Mji wa Gotland yameendelea kuonesha mafanikio makubwa katika sekta za Elimu, Maendeleo ya Jamii na Afya. Pia alichukua fursa hiyo kumweleza kuwa kwa upande wa Elimu, Shule ya Sekondari Kibaha imekuwa ya kwanza Kitaifa  kwa Shule za Sekondari za Serikali  katika mitihani ya Kidato cha nne kwa mwaka 2016.

Aidha, ugeni huo ulipata nafasi ya kupanda miti katika hifadhi ya miti ya Bertil Merlin na baadaye walipata fursa ya kukagua  mtambo wa hifadhi ya maji wa  SEK ambapo Mkadiriaji Majenzi Bw. Freddy Kambi alimweleza  Mhe. Meya na msafara wake kuwa mradi wa hifadhi wa maji ulipata ufadhili kutoka Mji wa Gotland Sweden mwaka 2009 na umeleta mafanikio makubwa kwani umewezesha kiasi cha maji kilichokuwa kikipotea kupungua kutokana na ukarabati  wa mabomba chini ya mradi huo. Msafara wa Mhe. Meya unaendelea na ziara katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha.