Habari
NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI ATEMBELEA KIBAHA SEKONDARI

NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI ATEMBELEA KIBAHA SEKONDARI
TAREHE 4 FEBRUARI,2020
NA; LUCY SEMINDU
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia elimu Mhe. Gerald Mweri ametembelea Shule ya Sekondari Kibaha kuona maendeleo ya ukarabati ambapo Serikali ya awamu ya tano imetoa kiasi cha bilioni 1.1 kwa ajili ya ukarabati huo.
Amesifu kazi iliyokwishafanyika na ameutaka uongozi wa shule kuhakikisha wanafunzi wanazingatia suala la usafi. Pia amewataka walimu kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku Serikali ikiendelea kutatua changamoto zao.
Baadaye alikuwa na kikao na Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari za Wilaya ya Kibaha ambapo alichukua fursa hiyo kumpongeza bw. Robert Shilingi kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha.