Habari

SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LATARAJIA KUWA NA UHUSIANO NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM OF AGRICULTURAL SCIENCES


SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LATARAJIA KUWA NA UHUSIANO NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM OF AGRICULTURAL SCIENCES

JANUARI 4, 2017

Shirika la Elimu kibaha linatarajia kuwa na uhusiano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam of Agricultural Sciences ambao utahusisha wanafunzi kutoka Chuo hicho  kuweza kuja  katika Shirika la Elimu Kibaha SEK kufanya tafiti mbalimbali za kilimo, mifugo, ufugaji nyuki na ufugaji wa samaki yaani  mafunzo kwa vitendo na utafiti.

Hayo yameeleezwa na Prof John Machiwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam College of Agricultural Sciences  alipofanya mazungumzo ya awali na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Bw. Robert Shilingi.

Profesa John Machiwa amesema College ya Agculturual Sciences kimeanzishwa hivi karibuni na kinatoa mafunzo ya shahada katika Beekeeping Science and Technology, Agricultural Engineering and Mechanization, Food Science and Technology and Agricultural and Natural Resources Economics and Business.

Amesema kwa kuwa wana changamoto ya eneo  kwa ajili ya wanafunzi wao kufanya tafiti na mafunzo kwa vitendo Shirika la Elimu Kibaha litakuwa ni eneo la msaada mkubwa kwa shughuli hiyo.

Aidha ,Ugeni huo ulipata fursa ya kutembelea katika eneo la Organia kuona uzalishaji kuku wa kisasa, Shamba darasa la mifugo ADF kuonakuona ufugaji wa sungura , bata na nguruwe pamoja na Shamba darasa la kilimo cha bustani za mbogamboga, maembe na ufugaji wa nyuki. Ushirikiano baina ya Taasisi husaidia kuchochea maendeleo.