Habari

SHIRIKA LAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI YA UMMA KWA KUPOKEA MAONI KUTOKA KWA WAFANYAKAZI


SHIRIKA LAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI YA UMMA KWA KUPOKEA MAONI KUTOKA KWA WAFANYAKAZI

 Na: Lucy Semindu – Shirika la Elimu Kibaha

Tarehe 22 Juni, 2017

Wiki ya Utumishi wa Umma huadhimishwa kila mwaka nchini Tanzania. Kwa kawaida kila tarehe 16 hadi 23 ya kila mwaka watumishi wa Umma hupata fusa ya kuonesha kazi wanazozifanya na kutoa maoni namna ya kuboresha Utumishi mahala pa kazi.

Leo Watumishi wa Shirika la Elimu wamepata fursa hiyo muhimu ya kutoa maoni ili kuboresha baadhi ya mambo katika Utumishi wa umma. Mratibu wa ukusanyaji maoni ya watumishi Bi Rose Mtei amesema kuwa mwaka huu watumishi wa Shirika la Elimu Kibaha kutoka Idara  mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kutoa maoni.

Shirika la Elimu Kibaha lilianzishwa mwaka 1973 na toka wakati huo limekuwa likijihusisha na mapambano ya maadui watatu wa taifa ambao ni Ujinga ,maradhi na umasikini.

Katika Kupambana na adui ujinga Shirika limejikita katika kutoa Elimu kuanzia shule ya awali mpaka Sekondari ikiwemo Shule ya Sekondari Kibaha inayofanya vizuri Kitaifa  katika mitahani ya kidato cha nne na kidato cha Sita.

Katika kupambana na adui maradhi, Shirika la Elimu linaendelea kutoa huduma ya afya kupitia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi ikiwemo kutoa mafunzo kwa vitendo ambapo kwa sasa inapokea wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma , Chuo Kikuu cha Kariuki, Chuo Kikuu cha Kariuki na Chuo cha Mtakataifu Joseph. Pia kupitia Chuo Kishirki cha Sayansi na Utabibu (KCOHAS)   mafuzo yanatolewa kwa madakari kwa ngazi ya diploma , manenesi, Wataalaam wa Maabara na Wafarmasia.

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (KFDC) kipo kwa ajili ya kupambana  na adui umasikini  ambapo Chuo hiki kimekuwa kikitoa mafunzo ya ufundi wa aina mbalimbali  na mafunzo ya ujasiriamali ambapo inawawezesha vijana kujiari na hivyo kujikwamua kiuchumi.