Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

MAFUNZO YA MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLAN) YAFUNGULIWA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA (KEC).

Imewekwa: 25 Aug, 2025
MAFUNZO YA MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLAN) YAFUNGULIWA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA (KEC).

MAFUNZO YA MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLAN) YAFUNGULIWA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA (KEC)

Kibaha, 25 Agosti 2025

— Mafunzo ya Mpango Mkakati (Strategic Plan) kwa viongozi wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC) yamefunguliwa rasmi leo tarehe 25-29, Agosti 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa KEC, Bw. Khalfan Feruz.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Bw. Khalfan aliwataka washiriki kuyachukulia kwa uzito mkubwa, akieleza kuwa Mpango Mkakati ni nyenzo muhimu katika kufanikisha malengo ya shirika kwa ufanisi, uwazi na tija.

“Mafunzo haya yatatusaidia kupanga kwa umakini shughuli za shirika letu, kuweka vipaumbele sahihi, na kupima maendeleo kwa njia yenye uwazi zaidi,” alisema Bw. Feruz.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuleta uelewa wa pamoja juu ya dira, malengo, na mikakati ya utekelezaji ndani ya KEC kwa kipindi kijacho.

Washiriki wa mafunzo wanatoka idara mbalimbali ndani ya Shirika la Elimu Kibaha, na mafunzo yanatarajiwa kuendelea kwa muda wa wiki moja.