SERIKALI KUBORESHA UTOAJI WA ELIMU SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA.
SERIKALI KUBORESHA UTOAJI WA ELIMU SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA.
Imewekwa: 01 Sep, 2025

Serikali imesema itaboresha miundombinu ya utoaji wa elimu katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha, Shule ya Sekondari Tumbi na Shule ya Msingi, zinazomilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha (KEC).
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu, Elimu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Atupele Mwambene wakati alipofanya ziara ya siku moja kupata taarifa ya utoaji wa elimu kupitia shule na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha.
Bw. Mwambene amesema Serikali itaboresha Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha kwa kukiwezesha kuwa na vifaa vya kisasa vya kufundishia pamoja na mahitaji mengine muhimu.