Habari

MKUU WA MKOA WA PWANI ASIFU JUHUDI ZA MAENDELEO SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA



MKUU WA MKOA WA PWANI ASIFU JUHUDI ZA MAENDELEO SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA

Ni katika miradi ya kuku wa kisasa, Ujenzi wa maabara na techolojia ya ukusannyaji mapoto ya Hospitali

 Kibaha Agosti 12,2015

Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhe. Evarist Ndikilo  amesifu mradi wa Organia ambao utakuwa ukizalisha kuku kwa njia ya technolojia ya kisasa. Kiwanda hicho cha uzalishaji wa kuku ni cha kwanza kwa aina yake Afrika Mashariki na Kati. Mradi huo unaweza kuajiri zaidi ya watu 1200 na kwamba utaongeza mapato kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha.

Aidha,amesifu fursa ya wajasiriamali wadogo kuweza kunufaika na mradi huo.kwani watapewa Chakula cha kuku ,mafunzo ,dawa na soko la uhakika kwani kiwanda hicho kitanunua kuku watakaozalishwa

Mhe. Ndikilo amesema kiwanda cha kuku cha Organia , kila mwaka kitahitaji zaidi ya maharage ya soya na zaidi ya  tani 8000 za mahindi ya njano. Hivyo hii ni fursa kwa wakulima wa Tanzania kuweza kunufaika. Amesifu mpango wa kuendeleza ardhi kwa kujenga nyumba za Watumishi na ameagiza ujenzi wa nyumba hizo uanze mara moja.

Kuhusu Mabara amesifu ujenzi wa maabara ya kisasa na ni ya mfano wa kuigwa kwa shule nyingine za Mkoa wa Pwani.

Akielezea mafanikio ya Shirika kwa Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha Dtk. Cyprian Mpemba amesema Shirika limepiga hatua kubwa ya kimaendeleo,aliitaja miradi ilionesha mafanikio ni pamoja na Kiwanda cha kuzalisha kuku cha kisasa kinachojengwa na Kampuni ya Organia kutoka Misri,mfumo wa kielectroniki wa ukusanyaji mapato ya hospitali,na mradi wa nyumba za makazi za watumishi zitakazojengwa na Kampuni ya Watumishi Housing limited.

Alifafanua kuwa mradi huo wa Nyumba za kisasa za watumishi zitakopeshwa kwa watumishi wa umma na kwamba itakuwa ni mkombozi kwa watumishi wa Umma, kwani itawahakikishia kupata nyumba bora za kisasa. Kuhusu Mfumo wa ukusanyaji mapato alisema tayari wameingia mkataba na Chuo Kikuu cha Mzumbe pamoja na kampuni ya BCX  na sasa mfumo huo ambao awali ulijulikana kwa jina la 4pay unaitwa GOT-HOMIS

 Shirika la Elimu Kibaha lilianza miaka ya sitini likiwa na misingi ya kupambana na maadui watatu ambao ni Ujinga, Umasikini na Maradhi.