Habari

WAHITIMU CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI KIBAHA WAPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI


WAHITIMU CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI KIBAHA WAPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

 Kibaha – 25, Novemba,2O15

Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi  Kibaha (KFDC) wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali katika ukumbi wa chuo hicho ujulikanao kwa jina la Ukumbi wa Twiga. Akitoa mafunzo hayo Meneja wa Mifugo wa Shirika la Elimu Kibaha Bw. Damas Msaki amesema kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa.

Alifafanua kuwa mafunzo hayo yanelenga kuandaa vijana waweze kupambana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira. Pia  amesema mafunzo hayo  yatawafanya vijana hao kuweza kugeuza changamoto za mitaani kuwa fursa kwa kuandaa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.

Pia wamepatiwa elimu ya jinsi ya kuunda vikundi ,sifa za wanachama ,sifa za vikundi na wajibu wa wanachama. Sanjari na hilo wamejifunza jinsi ya kuwa  wajasiriamali na namna bora ya kuhudumia wateja.  Sekta ya ujasiriamali imekuwa ikitoa ajira kwa watu wengi nchini.