Habari

WANAFUNZI WA VYUO VYA SHIRIKA LA ELIMU WACAHANGIA DAMU


WANAFUNZI WA VYUO VYA SHIRIKA LA ELIMU WACAHANGIA DAMU.

Na Lucy Semindu

22 Novemba,2017


Wanafunzi wa Vyuo vya Shirika la Elimu Kibaha wamejitokeza kwa hiari kuchangia damu kwa ajili ya wangonjwa wenye uhitaji mkubwa wa damu. Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kitengo cha damu salama katika Hospitali ya Tumbi Bw.  Oswald Maura wakati wanachuo hao walipochangia damu kwenye Kitengo cha damu salama cha Hospitali ya Tumbi.

Wanafunzi hao wanatoka katika Chuo cha Utabibu cha KCOHAS na Chuo cha Maendeleo ya Jamii KFDC. Kwa mujibu wa Ndugu Oswald Maura Kitengo cha damu salama kinatarajia kukusanya kiasi cha Unit 100 za damu katika zoezi hili la uchangiaji damu litakaloisha Ijumaa tarehe 24, Novemba,2017.

Ameeleza kuwa kwa kawaida Kitengo kinategemea wachangiaji wa damu kutoka misikitini,makanisani, Shule za Sekondari ,Vyuo na kwenye makongamano mbalimbali. Amesema mahitaji ya damu katika Hospitali ya Tumbi ni kati ya Unit 6 mpaka  8 kwa siku huku mahitaji ya mwezi yakifika kati ya Unit 180 mpaka 240.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi imekuwa ikipokea wagonjwa wengi wenye uhitaji wa damu hasa wanaotokana na ajali za barabarani.