Habari

​Watahiwa 155 wafaulu kidato cha sita kibaha Sekondari 2022


Shule ya Sekondari Kibaha (KSS) imefanikiwa kushika nafasi ya pili kimkoa kati ya shule 33 za Mkoa wa Pwani na nafasi ya 33 kitaifa kati ya shule 644.

Matokeo hayo yametangazwa leo na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) ambapo watahiniwa wote 155 wamefaulu kwa madaraja tofauti; wakiwemo watahiniwa 110 daraja la kwanza, 39 daraja la pili na sita daraja la tatu.

Ufaulu huu ni jitihada za uongozi wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC) kwa kushirikiana na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha.

Shule 10 zilizoongoza kwa ufaulu kidato cha sita nchini mwaka 2022 ni Kemebos Sekondari, Kisimiri Sekondari, Tabora Boys Sekondari, Tabora Girls Sekondari, Ahmes Sekondari, Dareda Sekondari, Nyaishozi Sekondari, Mzumbe Sekondari, Mkindi Sekondari na Ziba Sekondari.