Wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Kibaha wakiwa katika picha ya pamoja kama sehemu ya kumbukumbu ya safari yao ya masomo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC) wakiwa katika mahafali ya 57 ya wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2025 wa Shule ya Sekondari Kibaha
Wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Kibaha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeri rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Abdul Mombokaleo (katikati).
Mabalozi wa nchi nne za kinodiki, Sweden, Norway, Denmark na Finland wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Elimu Kibaha Pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kibaha wakati mabalozi hao walipotembelea Shirika la Elimu Kibaha (KEC).
Wanafunzi wa darasa la saba kutoka Shule ya Msingi Tumbi wakielezea kwa umahiri mada kuhusu damu, wakati wa mahafali yao yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo.
Bw. Silvanus Nyoni akitoa mafunzo kuhusu masuala ya maktaba kwa watumishi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha waliotembelea Shirika la Elimu Kibaha.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Robert Shilingi akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Juma Messos wakati alipotembelea Banda la Shirika la Elimu Kibaha kwenye Viwanja vya John Malecela jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Shiika la Elimu Kibaha katika maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane 2025 yaliofanyika Viwanja vya John Malecela jijini Dodoma.