Habari

Kumbukizi ya Miaka Hamsini ya Shirikala Elimu Kibaha yafana


Kumbukizi ya Miaka Hamsini ya Shirika la Elimu Kibaha yafana

Tarehe 10/01/2020

Na: Lucy Semindu – Kibaha

Shirika la Elimu   limetimiza miaka hamsini toka shirika hili lilipokabidhiwa rasmi kwa Serikali ya Tanzania tarehe 1/01/1970 . Shirika hili awali lilikuwa likijulikana kama Tangayika Nordic Project toka mwaka 1963 ambapo Hayati Mwalimu Nyerere na Rafiki zake toka nchi za Nordic walianzisha mradi huu ambao lengo lake ni kupambana na maadui wakubwa watatu ambao ni Ujinga, Maradhi na Umasikini.

Sherehe hizi ziliadhimishwa kwa kuwa na maonesho ya bidhaa na kazi mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Elimu na wadau wake na kuhitimishwa tarehe 10/01/2020 ambapo mgeni rasmi alikuwa  ni Mhe. Selemani Jafo Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi.

Mhe. Jafo amekabidhi tuzo mbalimbali za Heshima na Uongozi uliotukuka Miongoni mwa Viongozi waliopata tuzo hizo ni pamoja na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa  muasisi wa Shirika la Elimu  Kibaha kwa kupambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni ujinga ,maraddhi na umasikini, Rais Mtaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwa mwanafunzi wa kwanza wa Shule ya Sekondari Kibaha kufika nafasi ya juu katika uongozi wa Umma.

Hayati Bertil Merlin ambaye anatokea Sweden ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Kwanza na wengine ni Hayati Ferdinand Swai kwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Elimu aliyehudumu kwa miaka mingi. Mwingine ni Profesa Sarungi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani katika miaka ya themanini alijitolea japo alikuwa Mkuu wa Mkoa alifanya kazi ya kutoa huduma kwa wahanga wa ajali katika Hospitali ya Tumbi. Pia watumishi waliofanya kazi kwa zaidi ya miaka arobaIni walipokea tuzo.

Sherehe Hizi zilishehereshwa na Brass band,jazz band, muziki  ,ngoma na kwaya kwa kweli shughuli ya miaka hamsini ya Shirika la Elimu Kibaha ilifana sana.