Habari

Bodi Mpya ya Shirika la Elimu Kibaha yazinduliwa


Bodi Mpya ya Shirika la Elimu Kibaha yazinduliwa
 Na Lucy Semindu 
Tarehe 27 Maei,2020 
Bodi hiyo iliyozinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo ambapo ameiagiza Bodi ya Shirika la Elimu Kibaha kutumia rasilimali za Shirika kujiimarisha kiuchumi. Mhe Jafo ametoa agizo hilo wakati anazindua bodi mpya inayoongozwa na Profesa Raphael Chibunda. Katika maelezo yake Mhe. Jafo amesema Shirika limekuwa na rasilimamli nyingi ikiwemo ardhi kubwa .AmeItaka Bodi hii mpya kutumia rasilimali ardhi kupata wawekezaji watakaowekeza kwenye ardhi hiyo. Mhe Jafo ameonya kuwa uwekezaji utakaofanywa uwe wa kuleta tija kwa Shirika na Taifa kwa ujumla. Sanjari na hilo ameitaka bodi hii mpya kuendeleza falsafa iliyoanzishwa na Hayati Mwalimu Nyerere ya ambayo ni kupambana na ujinga ,maradhi na umasikini. Mhe Jafo ameipongeza Shirika kupitia Hospitali ya Tumbi kwa kuwa wabunifu na kutengeneza maji tiba ambayyo imeisaidia Serikali kupunguza gharama za kuagiza maji hayo. Pia ameipongeza Shule ya Sekondari ya Kibaba kwa kuendelea kufanya vizuri pamoja na Chuo cha KFDC. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Hiyo Profesa Raphael Chibunda amesema bodi yake itatekeleza maagizo yote aliyotoa. Shirika la Elimu Kibaha lilianza rasmi mwaka 1970 baada ya Tanzania kupokea mradi wa Tanganyika Nordic Project.