Habari
CHUO CHA MAENDELEO YA JAMIII KIBAHA
CHUO CHA MAENDELEO YA JAMIII KIBAHA
- Ni Kituo cha kuleta matumaini mapya kwa vijana
Oktoba 27, 2016
Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CHA KFDC) cha Shirika la Elimu Kibaha ni chuo cha kuleta matumaini mapya kwa vijana . Hayo yamesemwa na Bw. Sixbert Luziga wakati wa mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika leo katika viwanja vya KFDC Shirika la Elimu Kibaha
Katika hotuba yake kwa wahitimu wa Chuo hicho Bw. Luziga amesema Chuo hicho kimekuwa ni cha msaada sana katika kupambana na umasiki miongoni mwa vijana. Awali alikagua maonesho ya fani mbalimbali zinazofundishwa chuoni hapo ambayo ni pamoja na Kitengo cha uyeyushaji vyuma (welding), kilimo na mifugo, na ufundi bomba ,ushonaji na vitengo vingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Bi Anne Kuoko amesema chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1964 kikiwa ni kituo cha mafunzo ya kilimo kimepitia hatua nyingi za kuendelea kutoa ellimu ya kupambana na umasikini kwa kuwezesha vijana kupata mafunzo yanayowawesha kujitegemea na hivyo kupambana na umasikini
Awali Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Maendeleo ya Jamii Shirika la Elimu Kibaha Bw. Annathe Nnko amesema Chuo hicho kimeweza kuibua vipaji mbalimbali miongoni vya vijana ambavyo vimewezesha kuweza kutumia vipaji hivyo kujitegemea wamalizapo mafunzo chuoni.
Shirika la Elimu kibaha lilianzishwa rasmi mwaka 1970 ikiwa na malengo matatu amabayo ni kupambana na ujinga,maradhi na umasikini