Habari

DKT. CYPRIAN MPEMBA AWAPONGEZA WATUMISHI WA SEKONDARI YA KIBAHA


DKT. CYPRIAN MPEMBA AWAPONGEZA WATUMISHI WA SEKONDARI YA KIBAHA

Na Lucy Semindu  - Kibaha

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Dkt. Cyprian Mpemba amewapongeza watumishi wa Sekondari ya Kibaha. Pongezi hizo zimetolewa jana wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza watumishi hao kwa kuiwezesha  Shule hiyo kupata ushindi wa pili kitaifa katika mitihani ya kidato cha nne  mwaka 2015 kwa Shule za Serikali.

Aidha, Dkt Mpemba amesema amefarijika sana na matokeo hayo na kwa kweli walimu na watumishi hao “wamemtoa kimaso kimaso”kwa kuiwezesha Sekondari ya Kibaha kupata ufaulu huo mkubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Elimu Shirika la Elimu Kibaha Bw. Robert Shilingi amesema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo walimu na watumishi wameiwezesha shule hiyo kung’ara kitaifa kwa Shule za Serikali .

Awali akielezea mafanikio ya kitaaaluma ya Shule hiyo ,Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Bw. Chrisdom ambilikile amesema Shule yake imekuwa ya pili Kitaifa kwa Shule za Serikali na kwa Shule zote za Binafsi na Serikali ilishika nafasi ya 69 Kitaifa .

Hata hivyo amesema tayari wamepanga na wameanza kutekeleza mikakati itakayoiwezesha Shule yake kuweza kushika  nafasi ya kumi bora kitaifa kwa mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2016.

Kibaha Sekondari ni moja ya Shule za Serikali inayofanya vizuri kitaaluma.