Habari
HELPING HANDS YOUTH FOUNDATION AFIRICA YATOA MSAADA WA KIPAZA SAUTI KWA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

Oktoba 17,2016
Shirika lisilo la Kiserikali la Helping hands Youth foundation Africa limetoa msaada wa kipaza Sauti kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Kibaha.Tukio hilo lililosisimua Walimu wa Shule ya Kibaha limetokea leo katika Ofisi ya Walimu ya Shule hii.
Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi MtendajI wa Asasi hiyo ambaye pia ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha Bw. Steven Msama amesema kuwa kama mwanafunzi wa Kibaha Sekondari ameona changamoto kubwa ya mawasiliano wanayopata Walimu na Wanafunzi wakiwa katika mkutano na mikusanyiko shuleni.
Bw.Msama ameeleza kuwa aliwasilisha ombi la kuchangia kipaza sauti kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Kibaha ,ombi ambalo lilikubaliwa na wanachama wake. Ameeleza Asasi ya Helping hands Youth foundation Africa yenye makao yake jijini Dar es Salaam ina lengo la kuwawezesha na kutoa elimu kwa vijana kuhususiana na masuala mbalimbali kama vile kuinua vipaji ,kupambana na vitendo vilivyo nje ya maadili miongoni mwa vijana.
Kwa Upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibaha Bw. Crisdom Ambilikile amemshukuru Bw. Msama kwa msaada huo wa kipaza sauti na kwamba kitasaidia katika mawasiliano shuleni . Amesema licha ya uchanga na changamoto zinazoIkabili Taassi hiyo amejitokeza kuchangia. Amewataka wafadhili wenye nia ya kuendeleza vipaji na malezI kwa vijana kujitokeza kuisadia Taasisi hiyo.