Habari

HOSPITALI YA TUMBI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA TIBA KUTOKA COCA COLA AMERIKA



HOSPITALI YA TUMBI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA TIBA KUTOKA COCA COLA AMERIKA

Tarehe 2 Mei,2016

Hospitali ya Tumbi imepokea msaada wa vifaa tiba kutoka Kampuni ya Cocacola ya Amerika kupitia MSD wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 10, hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Elimu Kibaha Bi. Lucy Semindu wakati  msaada huo ulipopokelewa leo katika Hospitali ya Tumbi .

Aidha, Bi Lucy amesema kuwa msaada huo una manufaa makubwa kwa Hospitali ya Tumbi ikizingatiwa Hospitali hiyo ilikuwa ina upungufu wa vifaa tiba. Alitaja baadhi ya vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na:gloves,mabomba ya sindano, kiti cha kukalia, mashine ya kupimia BP, makoti maalum wakati wa upasuaji,  meza ya kumkagua mgonjwa,mataulo, catheter, kifaa cha mazoezi ya viungo ,nyuzi kwa ajili ya kushona wakati wa upasuaji na vifaa vingine.

Bi.Lucy Semindu kwa niaba ya Uongozi wa Shirika la Elimu Kibaha  ameishukuru Kampuni ya Cocacola ya Amerika kwa msaada huo mkubwa kwani utaiwezesha Hospitali ya Tumbi kutekeleza vyema majukumu yake ya kila siku.Kampuni ya Cocacola ya Amerika ni moja ya mashirika makubwa duniani ambayo hutoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali pale vinapohitajika.