Habari
SIKU YA TAALUMA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA KIBAHA YAFANA

SIKU YA TAALUMA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA KIBAHA YAFANA
- WALIFANYA VIZURI KATIKA NJANJA MBALIMVBALI WAKABIDHIWA VYETI
Tarehe: 7/08/2019
NA: LUCY SEMINDU- KIBAHA
Siku ya taaluma Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha yafana. “Siku hii imeadhimishwa mwaka huu na itakuwa endelevu” hayo yamesemwa na Mkuu wa Shule hiyo Bi Felister Mathias wakati akitambulisha siku hii rasmi kwa wanafunzi,wazazi ,wageni waalikwa na wadau mbalimbali wa elimu.
Siku hii ilitanguliwa na maonesho ya taaluma ambapo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha walionesha umahiri mkubwa katika taaluma.
Mgeni rasmi katika siku hiyo muhimu alikuwa ni Diwani wa Picha ya Ndege Mhe. R.J Machumbe ambaye alifarijika sana na vipaji walivyonavyo wanafunzi hao ,kwani yeye mwenyewe alitoa zawadi ya fedha kiasi cha shilingi elfu kumi kwa kila mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo kwa mwaka 2018.
Sherehe hizi zilipambwa kwa nyimbo,maigizo,ngonjera na midahalo mbalimbali. Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washindi kitaluuma kwa katika darasa ,masomo,nidhamu,mazingira ,unadhifu na kwa wanafunzi walioonesha bidii ya kuvuka daraja moja kwenda jingine. Washindi walikabidhiwa vyeti vya kuwatambua.
Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha ni miongoni mwa Shule za Sekondari za Mkoa wa Pwani ambazo zinafanya vizuri kitaaluma.