Habari

Timu za Shirika la Elimu Kibaha Zangara


Timu ya soka ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KFDC) na timu ya netiboli ya chuo hicho ambazo zinamilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha (KEC) zimepata ushindi mnono katika mechi za kirafiki zilizochezwa viwanja vya Shirika hilo.

Mechi ya soka ilikuwa ni kati ya KFDC na Timu ya Njuweni wakati Timu ya Netiboli ya KFDC ilikipiga na Timu ya Netiboli ya Njuweni zote kutoka mkoani Pwani.

Timu ya soka ya KFDC ilifanikiwa kuichabanga Njuweni mabao 4-0 katika mchezo mkali uliovutia, mashabiki wa pande zote mbili ambao walikuwa wakihamasisha ushindi mwanzo mwisho.

Mabao ya wenyeji KFDC yaliwekwa nyavuni na Babuali Mashaka ambaye alifunga goli la kwanza na la nne, goli la pili Athumani Seif maarufu Ochu na goli la tatu Paschal Lyuba maarufu Duchu.

Wakati timu ya mpira wa miguu ya KFDC ikitakata katika uwanja wao wa nyumbani, dada zao wawaliwamiminia mvua ya magoli 40-4 Timu ya Netiboli ya Njuweni bila huruma.

Timu za Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha, zilipewa zawadi ya jezi pamoja na mpira. Mechi hizo zilifadhiliwa na Vodacom Tanzania.