Habari

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU ATHARI YA RUSHWA


WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU ATHARI YA RUSHWA

Tarehe 19/09/2019

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa B.Merlin yalifunguliwa rasmi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Bw. Robert Shilingi na baadaye mratibu wa mafunzo hayo ambaye ni Meneja wa Utawala bw. Lusungu Nyagawa alimkaribisha Mtoa mada kutoka ofisi ya Takukuru Mkoa wa Pwani Bw.Hassan Chamsama kutoa maada hiyo.

 Bw. Chamsama alifafanua kuwa rushwa ni kitendo ambacho mtu anakifanya bila kufuata utaratibu kwa lengo la kujipatia manufaa yake binafsi au ya mtu mwingine.

 Aliwakumbusha watumishi kuwa waadilifu wanapofanya kazi za Serikali na kama kuna dalili yoyote ya rushwa mahali pa kazi wasisite kutoa taarifa kwa mamlaka husika kupitia namba 113 kwa kupiga simu au kuandika ujumbe mfupi.Amesisitiza watumishi kujiepusha na vitendo vitakavyopelekea kutenda kosa la rushwa.

 Vifungu ambavyo vimesisitizwa ni kifungu no 22 ambacho kinahusu udanganyifu wa nyaraka mfano kumdanganya muajiri katika marejesho ya fedha (retirement). Kifungu cha 28 ambapo mtu anatumia mamlaka yake kufanya ubadhirifu au matumizi ya pesa kinyume na ilivyopangwa na kifungu cha 31 cha matumizi mabaya ya madaraka.

 Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ilianzishwa kwa lengo la kuzuia na kupambana na rushwa na ina infanya kazi kwa kutoa elimu kwa wananchi ,kufanya utafiti na ukaguzi wa miradi mbalimbali kuona kama inatekelezwa kama ilivyokusudiwa.