Habari

Wajumbe dawati la jinsia KEC wapewa mafunzo


Wajumbe wa dawati la jinsia la Shirika la Elimu Kibaha (KEC) leo Jumatano tarehe 26/07/2023 wamepatiwa mafunzo ya namna ya uendeshaji wa dawati hilo mahali pa kazi.

Akitoa mafunzo hayo yenye lengo la kuimarisha utendaji kazi wa dawati hilo, Bi. Feliciana Mmasy ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii amewataka wajumbe hao kuisaidia menejimenti ya KEC kuyatambua na kuyashughulikia maswala mbalimbali ya watumishi yanayolenga mambo ya jinsia, kutoa elimu kwa watumishi kuhusu maswala ya jinsia na kuhakikisha kwenye miradi na shughuli zote zinazofanyika KEC maswala ya jinsia yanazingatiwa.

Dawati la jinsia eneo la kazi ni wawakilishi wa watumishi wengine katika taasisi wanaohakikisha usawa wa kijinsia unazingatiwa katika maeneo ya kazi. Dawati hilo la KEC lilianzishwa mwaka 2018 na lina jumla ya wajumbe 12 ambao wanawakilisha vitengo na kurugenzi zilizopo katika shirika hilo

Lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha utendaji kazi wa dawati la jinsia la KEC na mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa maktaba ya umma iliyopo kwenye shirika hilo.