Habari
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA WACHANGIA DAMU KWA AJILI YA HOSPITALI YA TUMBI

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA WACHANGIA DAMU KWA AJILI YA HOSPITALI YA TUMBI
Na: Lucy Semindu Kibaha
Tarehe 19 Januari, 2017
Kitengo cha damu Salama cha Hospitali ya Tumbi leo wapo katika Shule ya Sekondari Kibaha ambapo wanafunzi wa Shule hiyo wanajitolea damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi wenye uhitaji mkubwa wa damu .
Kila mwaka wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kibaha wamekuwa na desturi ya kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa wanaokuja katika hospitali ya Tumbi .Shukrani zimwendee Mkuu wa Shule hiyo Bw. Chrisdom Ambilikile kwa kuhamasisha vijana hao kujitolea kwa maslahi ya Taifa.