Habari

Wanawake wa Shirika wang'ara Siku ya Wanawake Duniani


Watumishi wanawake wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC) zaidi ya 60 wameshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika kiwanja cha Mwanakalenge, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Machi 8 2023.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okashi akimuwakilisha m

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mhe. Okashi amewapongeza wazazi kwa kuhamasika kuwapeleka watoto wa kike shuleni na kusababisha uandikishaji kuongezeka.

"Uandikishwaji wa watoto wa kike ni mkubwa, hii inatokana na watoto wa kike kuzaliwa kwa wingi na wazazi kuhamasika kuwasomesha watoto wa kike tofauti na zamani. Hii imetokana na Serikali yetu kuwekeza katika sekta ya elimu, watoto wengi wa kike watanufaika na uwekezaji huo ndiyo maana kuna msemo usemao ukielimisha mtoto wa kike umeelimisha Taifa zima," amesema Mhe. Okashi.

Pia, Mhe. Okashi ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wanawake wote kufanya shughuli za maendeleo ili kutoa mchango katika maendeleo endelevu ya Taifa.

Maadhisho hayo yameenda sambamba na wanawake wajasiriamali kuonesha bidhaa mbalimbali wanzotengeneza na kuuza.

Pia wanawake waliohudhuria walipata elimu juu ya ukatili wa kijinsia na namna ya kupambana nao iliyotolewa na dawati la jinsia Mkoa wa Pwani.

Maadhimisho haya hufanyika kila mwaka tarehe 08 Machi, na kauli mbiu ya mwaka huu ni Ubunifu na mabadiliko ya Teknolojia, Chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.